Stanislaus Kostka
From Wikipedia, the free encyclopedia
Stanislaus Kostka (Rostkowo, leo nchini Polandi, 28 Oktoba 1550 – Roma, Italia, 15 Agosti 1568[1]) alikuwa kijana mnovisi katika shirika la Wajesuiti.
Ili kujiunga nalo alitoroka nyumbani na kwenda kwa miguu hadi Roma, alipopokewa na Fransisko Borja. Aliwahi kufariki dunia kutokana na uchovu katika kutoa huduma duni zaidi[2].
Tarehe 9 Oktoba 1605 alitangazwa na Papa Paulo V kuwa mwenye heri, halafu tarehe 31 Desemba 1726 akatangazwa na Papa Benedikto XIII kuwa mtakatifu.