Solomoni wa Bretagne
From Wikipedia, the free encyclopedia
Solomoni III wa Bretagne (kwa Kibretoni: Salaün; alifariki Bretagne, leo nchini Ufaransa, 25 Juni 874) alikuwa mfalme wa Bretagne kuanzia mwaka 857.
Ili kufidia uuaji wa ndugu yake alioufanya kanisani ili kujitwalia madaraka alijitahidi sana kuanzisha majimbo na monasteri na kudumisha haki.
Hatimaye alipofushwa na kuuawa na maadui wake kanisani vilevile[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[2].