Silvia wa Roma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Silvia wa Roma (520 hivi - 592 hivi) alikuwa mwanamke Mkristo, mama wa Papa Gregori I na mtoto mwingine asiyejulikana kwa jina [2].
Baada ya kufiwa mume wake, Gordiani (573), aliishi kama mmonaki wa Kibenedikto[3][4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, msimamizi wa wajawazito[5].