Salve Regina
From Wikipedia, the free encyclopedia
"Salve Regina" (tamka:ˈsalve reˈdʒiːna; maana yake: 'Salamu Malkia') ni utenzi wa Kikristo unaotumika katika liturujia ya Kanisa la Kilatini hasa kama antifona mojawapo ya kumalizia Sala ya mwisho nje ya Kipindi cha Pasaka. Kwa kawaida unatumika pia kumalizia sala ya Rozari[1].
Utenzi huo ulitungwa na mtu asiyejulikana[2] wa Ulaya katika Karne za Kati na ulitumika kwanza kwa lugha ya Kilatini, ingawa kuna tafsiri zake nyingi.