Salome (mke wa Zebedayo)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Salome (kwa Kiebrania: שלומית, Shelomit, kutoka mzizi שָׁלוֹם, shalom, yaani amani[1]) alikuwa mke wa Zebedayo na mfuasi wa Yesu Kristo pamoja na wanae Yakobo Mkubwa na Mtume Yohane, waliokuwa marafiki wakuu wa Yesu pamoja na mtume Petro.
Kwa msingi huo alithubutu kumuomba Yesu awape wanae nafasi mbili za kwanza katika ufalme wake ujao.
Anatajwa kati ya wanawake waliosimama chini ya Yesu msalabani (Mk 15:40; Math 27:56) na kati ya wale waliowahi kwenda kaburini Jumapili asubuhi na mapema (Mk 16:1)[2].
Pengine anadhaniwa kuwa na undugu na Bikira Maria, mama wa Yesu.[3]