Rosa Venerini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Rosa Venerini (Viterbo, leo mkoani Lazio, Italia, 9 Februari 1656 – Roma, 7 Mei 1728) alikuwa bikira maarufu kwa huduma yake katika malezi ya wasichana. Kwa ajili hiyo alianzisha shule ya kwanza kwa wasichana tu nchini Italia, halafu shirika la masista walimu linalodumu hadi leo. Alipofariki shule zake zilikuwa 40 tayari.
Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 4 Mei 1952, halafu Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 15 Oktoba 2006[1].