Raymond Aaron
From Wikipedia, the free encyclopedia
Raymond-Claude-Ferdinand Aron (14 Machi 1905 – 17 Oktoba 1983) alikuwa mwanafalsafa, mwanasosholojia, mwandishi wa habari na mtaalamu wa masuala ya siasa kutoka nchini Ufaransa.
Anafahamika pia kutokana na uhusiano wake wa muda mrefu wa kirafiki na wakati mwingine wa kiuhasama na Jean-Paul Sartre.[1]. Pia anafahamika zaidi kutokana na kitabu chake kilichotoka mwaka 1995, kilichofahamika kwa jina la The Opium of the Intellectuals.
Aron pia aliandika kwa undani kuhusu mada nyingine nyingi katika sosholojia, habari na filosofia. Akizungumzia kuhusu undani na ubora wa kazi za Aron, mwandishi na mwanahistoria James R. Garlan [2] ameandika kuwa, ijapokuwa anaweza kufahamika zaidi nchini Marekani, lakini Raymond Aron, anatajwa kuwa ni mtu maarufu sana miongoni wa wasomi wa nchini Ufaransa wa karne ya ishirini.