Petro wa Verona
From Wikipedia, the free encyclopedia
Petro wa Verona, O.P. (Verona, Veneto, 1206 ā Lombardia, 6 Aprili 1252) alikuwa padri wa Italia Kaskazini na mmojawapo kati ya Wadominiko waliofia dini nchini mwake.
Wazazi wake walikuwa wafuasi wa Mani, lakini mwenyewe utotoni alijiunga na Kanisa Katoliki halafu ujanani Dominiko Guzman alimpokea katika shirika lake jipya.
Alijitosa kupambana na uzushi kwa kila njia.
Kama alivyotamani na kuomba, aliuawa na mzushi akiwa njiani kati ya Milano na Como. Kufani alikuwa akikiri imani sahihi[1]. Baadaye muuaji wake, Karino wa Balsamo, alitubu na kujiunga na utawa kama bruda, naye anaheshimiwa kama mwenye heri.
Petro anaheshimiwa kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Inosenti IV tarehe 9 Machi 1253, upesi kuliko mwingine yeyote[2].