Papa Benedikto V
From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Benedikto V alikuwa Papa kuanzia Mei 964 hadi tarehe 4 Julai 964 au 965[1]. Alitokea Roma, Lazio, Italia[2].
Jina lake la kuzaliwa halijulikani.
Alimfuata Papa Leo VIII akafuatwa na Papa Yohane XIII.
Alilazimishwa kujiuzulu na Kaisari Otto I wa Ujerumani aliyempeleka kwenda mji wa Hamburg alipofariki tarehe 4 Julai 966.