Oliva wa Palermo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Oliva wa Palermo (Palermo, Italia, 448 - Tunisi, Tunisia, 10 Juni 463) alikuwa msichana wa ukoo maarufu wa Palermo aliyepelekwa uhamishoni na Wavandali wa mfalme Genseriki na hatimaye kuuawa kwa kukatwa kichwa kwa sababu ya imani yake[1][2][3][4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu bikira mfiadini.