Olaf II Haraldsson
From Wikipedia, the free encyclopedia
Olaf II Haraldsson (kwa Kinorwe asili: Ólafr Haraldsson; pia Olave; 995 – 29 Julai 1030) alikuwa mfalme wa Norway kuanzia mwaka 1015 hadi 1028.
Mtu wa watu, alieneza katika ufalme wake imani ya Kikristo aliyoifahamu huko Uingereza, akapambana na Upagani kwa bidii hadi alipouawa na maadui waliomshambulia kwa upanga huko Stiklestad[1].
Mwaka mmoja baadaye alitangazwa na askofu Grimketel huko Nidaros (Trondheim) kuwa mtakatifu. Jambo hilo lilichangia sana uenezi wa Ukristo nchini, naye akawa kiini cha utambulisho wa taifa[2][3].
Mwaka 1164 Papa Alexander III alithibitisha utakatifu wake.
Pamoja na Wakatoliki na Waorthodoksi[4], baadhi ya Walutheri na Waanglikana pia wanamheshimu hivyo.[5]