Niseforo wa Konstantinopoli
From Wikipedia, the free encyclopedia
Niseforo I wa Konstantinopoli (kwa Kigiriki: Νικηφόρος Α΄, Nikēphoros I; Konstantinopoli, leo Istanbul nchini Uturuki, 758 hivi – Konstantinopoli, 5 Aprili 828) alikuwa mwandishi wa Kikristo wa Dola la Bizanti na Patriarki wa Konstantinopoli tangu 12 Aprili 806 hadi 13 Machi 815.[1][2]
Aliondolewa madarakani na kaisari Leo V na kupelekwa kuishi monasterini kwa sababu ya kutetea matumizi ya picha takatifu.
Huko aliendelea kuandika ili kutetea matumizi hayo[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.