Mzee Simeoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mzee Simeoni alikuwa mwanamume mwadilifu wa Yerusalemu (leo nchini Palestina/Israeli) katika karne ya 1 KK.
Ni maarufu hasa kwa kumpakata mtoto Yesu alipoletwa na wazee wake katika hekalu la Yerusalemu siku 40 tu baada ya kuzaliwa Bethlehemu.
Kadiri ya Injili ya Luka (2:25-35[1]) alikwenda kumlaki kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu aliyekuwa amemuahidia hatakufa kabla hajamuona Masiya.
Alipomtambua katika mtoto huyo alishangilia na kumsifu Mungu kwa wimbo maarufu alipomtangaza Yesu kuwa ndiye wokovu ulioandaliwa kwa mataifa yote.
Baada ya hapo alimtabiria Bikira Maria kwamba upanga utamchoma moyo kuhusiana na upinzani utakaompata mwanae.
Tangu kale anaheshimiwa na madhehebu mengi ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 2, 3[2] au 15 Februari.