Mkataba wa Schengen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mkataba wa Schengen (kwa Kiingereza: Schengen Agreement; kwa Kifaransa: Accord de Schengen) ni makubaliano ya kimataifa huko Ulaya ambayo yanalenga kukomesha udhibiti wa mpaka uliopo kati ya nchi na nchi na pia ushirikiano katika mipaka ya nje kwenye ardhi kavu na majini[1]. Haiathiri udhibiti wa forodha: hizo zinasimamiwa na Umoja wa Forodha wa Ulaya.
Jina linatokana na mji wa Schengen nchini Luxemburg ambako mapatano yale yalitiwa sahihi.
Raia wa nchi za wanachama wanaweza kusafiri bila vizuizi ndani ya eneo la Schengen bila kuomba visa au idhini ya makazi[2]. Raia wa nchi zilizo nje ya eneo la Schengen kwa kawaida hupokea "Viza ya Schengen", ambayo pia inawapa haki ya kukaa katika nchi zote wanachama.
Wakati wa kuvuka mipaka ndani ya eneo la Schengen, inahitajika pia kuwa na kitambulisho. Kwa raia wa eneo la Schengen ni kitambulisho halali au Pasipoti, kwa raia kutoka nchi zilizo nje ya eneo la Schengen pasipoti halali na, ikiwa ni lazima, viza.