Masimiano wa Ravenna
From Wikipedia, the free encyclopedia
Masimiano wa Ravenna (Pula, leo nchini Croatia, 499 - Ravenna, Emilia-Romagna, Italia, 22 Februari 556 hivi) alikuwa askofu wa 28 wa mji huo wa Italia Kaskazini akawa askofu mkuu wake wa kwanza kwa miaka kumi hadi kifo chake[1].
Alifanya vizuri uchungaji na alidumisha umoja wa Kanisa kwa kupinga Uario.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 22 Februari[2].