Margerita wa Cortona
From Wikipedia, the free encyclopedia
Margerita wa Cortona (Laviano 1247 – Cortona 22 Februari 1297) alikuwa mwanamke wa Italia aliyefanya toba katika Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko baada ya kuishi na mwanamume bila ndoa kwa muda wa miaka kumi.
Kwa kushtushwa sana na kifo cha ghafla cha huyo hawara wake, alifidia kwa malipizi makali dhambi za ujanani akazama katika mambo ya mbinguni kwa kujazwa na Mungu karama za pekee sana.
Papa Benedikto XIII alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Mei 1728.