Lusia Filippini
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lusia Filippini (Corneto-Tarquinia, Lazio, 16 Januari 1672 - Montefiascone, Lazio, 25 Machi 1732) alikuwa mwanamke wa Italia ya kati ambaye, kwa msaada wa kardinali Marcantonio Barbarigo, alianzisha shirika la Walimu wa Kikristo kwa ajili ya malezi ya wasichana na wanawake, hasa fukara[1].
Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Juni 1926 na mtakatifu tarehe 22 Juni 1930.