Lidia wa Thiatira
From Wikipedia, the free encyclopedia
Lidia wa Thiatira (au Ludia wa Thuatira; kwa Kiingereza Lydia of Thyatira; kutoka Kigiriki Λυδία, jina la mkoa wa Dola la Roma ulikokuweko mji wa Thiatira, katika Uturuki wa leo[1]) alikuwa mwanamke mfanyabiashara wa karne ya 1[2] ambaye kwanza aliongokea dini ya Uyahudi[3][4].
Mwinjili Luka katika Matendo ya Mitume (kitabu cha Agano Jipya la Biblia ya Kikristo) alisimulia habari zake; hivyo amekuwa mtu wa kwanza wa Ulaya ambaye anajulikana kwa jina kuwa aliongokea Ukristo[5]. Ni tunda ambalo Mtume Paulo alilichuma huko Filipi (Ugiriki Kaskazini)[6].
Madhehebu mengi yanamheshimu kama mtakatifu katika tarehe tofautitofauti[7][8][9][10][11][12][13]. Kwa Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini sikukuu yake ni tarehe 20 Mei[14] (awali 3 Agosti)[15].