Leonardo wa Portomaurizio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Leonardo wa Portomaurizio (Porto Maurizio, leo Imperia, 20 Desemba 1676 - Roma 26 Novemba 1751), alikuwa mtawa wa shirika la Ndugu Wadogo na padri wa Kanisa Katoliki kutoka Italia.
Ndiye tunda bora la Kirekebisho cha utawa wa Ndugu Wadogo kilichoanzia mjini Roma karne XVII.
Ni maarufu hasa kwa mahubiri yake ya wiki nzima (wiki za uamsho) aliyoyaendesha karibu mfululizo kati ya waamini wa Kanisa Katoliki nchini Italia, akisisitiza hasa ibada kwa mateso ya Yesu kwa kupitia vituo 14 vya njia ya msalaba.
Aliyeendesha wiki hizo mara 343, akiongozana kwa kawaida na mapadri 4 na bradha 1. Baada ya wiki mbili za mahubiri kulikuwa na wiki moja ya maungamo.
Katika miaka 44 aliokoa watu wengi ajabu, na kuinua hali ya roho ya mapadri wanajimbo na watawa katika Italia karibu nzima.
Ndiye mwenezaji mkuu wa Njia ya Msalaba, ibada iliyoanza kustawi katika karne XV ikiwa na vituo 7 hadi 37, mpaka ile ya 14 ilipopewa rehema ya pekee (1686) na hivyo kuenea popote.
Papa Pius VI alimtangaza mwenye heri, halafu Papa Pius IX akamtangaza mtakatifu tarehe 29 Juni 1867.