La Cristiada
From Wikipedia, the free encyclopedia
La Cristiada ni jina la Kihispania la vita vya Cristeros (1926-1929) vilivyotokea nchini Meksiko kati ya wakulima Wakatoliki na serikali ya nchi iliyotaka kutekeleza sheria dhidi ya uhuru wa dini.
Chinichini maaskofu waliunga mkono juhudi za waumini wao hata walipotumia silaha kutetea haki yao ya kuabudu kwa pamoja. Marekani ilifanya kazi ya upatanisho na mwishoni maaskofu walikubaliwa na serikali idhini kadhaa, hivyo vita vikaisha.