Kristina wa Bolsena
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kristina wa Bolsena (anajulikana pia kama Kristina wa Turo, au Kristina Mfiadini mkuu[1]) alikuwa mwanamke Mkristo wa karne ya 3 aliyefia dini yake.
Ingawa habari za maisha yake hazijulikani, tangu karne ya 4 anaheshimiwa huko Bolsena (Lazio, Italia)[2] na sehemu nyingine[3] kama mtakatifu bikira mfiadini[4][5].