Kisiwa cha Rubondo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kisiwa cha Rubondo ni kisiwa kimojawapo cha mkoa wa Geita, kaskazini mwa Tanzania, ambacho kinapatikana katika Ziwa Viktoria, ambalo ni ziwa la pili kwa ukubwa duniani, likiwa linazungukwa na nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda.
Ndipo ilipo hifadhi ya kisiwa cha Rubondo iliyoanzishwa huko kwa sababu kisiwa cha Rubondo ni makazi na mazingira muafaka ya kuzaliana samaki wakiwemo sato na sangara. Sangara huweza kuwa na ukubwa wa hadi kilo 100.
Fukwe za kisiwa hiki ni miongoni mwa makazi ya pongo na nzohe. Aidha hifadhi hii ni maskani makuu ya ndege na samaki kama zumbuli, chechele na taisamaki.
Mbali na ndege hao kisiwa hiki ni makazi ya aina nyingine nyingi za ndege wa majini na mimea kadhaa ambayo hutoa harufu nzuri ya kuvutia.
Wanyama wakazi wa hifadhi hii ni kama viboko, pongo, nzohe, fisi maji, mamba na pimbi ambao wanashirikiana makazi na wanyama waliohamishiwa katika hifadhi hii kama sokwe, tembo, mbega weusi na weupe na twiga.