Kipembezo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Katika utarakilishi, kipembezo (pia: pembezo[1]; kwa Kiingereza: peripheral) ni kitumi chote cha tarakilishi ambacho kinatumika ili kuingia na kuondoa taarifa kutoka tarakilishi.
Kuna aina kadhaa za vipembezo.
- Kitumi cha kuingia ambacho kinatuma data tarakilishi, kama kipanya, baobonye, kamera pembuzi au kitambazo.
- Kitumi cha kutolea ambacho kinatoa kitoleo cha tarakilishi, kama kichapishi, skrini au kipaza sauti.