Katharine Drexel
From Wikipedia, the free encyclopedia
Katharine Marie Drexel (26 Novemba 1858 – 3 Machi 1955) alikuwa mtawa wa kike na mwanzilishi wa shirika la Masista wa Ekaristi Takatifu (kwa Kiingereza Sisters of the Blessed Sacrament).
Jumuiya hiyo kwanza ililenga hasa kuwainua Wahindi Wekundu na Wamarekani weusi huko Marekani. Kwa ajili yao alitumia kwa ukarimu na upendo urithi wake mwenyewe.
Alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 20 Novemba 1988 na mtakatifu tarehe 1 Oktoba 2000.