Kartaki wa Lismore
From Wikipedia, the free encyclopedia
Kartaki wa Lismore (pia: Mo Chutu, Mochuda, Kartaki Kijana; Fingen, Ireland, 555 hivi - Lismore, Ireland, 14 Mei 639[1]) alikuwa padri aliyekwenda kuishi upwekeni miaka 14, halafu akajiunga na monasteri ya Bangor kabla ya kuanzisha ya kwake huko Rathin akiipatia kanuni mpya kwa lugha ya Kieire.
Mwaka 635 yeye na wanafunzi wake walifukuzwa huko na hatimaye akawa askofu wa kwanza wa Lismore[2] baada ya kuanzisha huko monasteri nyingine iliyovuta vilevile wafuasi wengi[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi[4] na Waanglikana kama mtakatifu.