Karoli wa Mlima Argus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Karoli wa Mlima Argus, C.P. (jina la kuzaliwa: Joannes Andreas Houben; Munstergeleen, Limburg, Uholanzi, 11 Desemba 1821 ā Harold's Cross, Dublin, Ireland, 5 Januari 1893) alikuwa padri Mpasionisti aliyefanya kazi huko Ireland.
Alipata sifa kubwa kutokana na huruma yake kwa wagonjwa[1][2] na wale waliohitaji ushauri nasaha, hasa katika kitubio[3].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 16 Oktoba 1988, na Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 3 Juni 2007.