Karitoni na wenzake
From Wikipedia, the free encyclopedia
Karitoni na wenzake Karito, Evelpisto, Gerasi, Peoni na Liberiani (walifariki Roma, Italia, kati ya 162 na 168) walikuwa wanafunzi sita wa Yustino ambao waliuawa pamoja naye kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya Dola la Roma[1][2].
Hati za mateso yao zimetunzwa hadi leo[3].
Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama watakatifu wafiadini.