Jumuiya ya Afrika Mashariki
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jumuiya ya Afrika Mashariki au Mtangamano wa Afrika Mashariki (kwa Kiingereza East African Community, kifupi EAC) ni muundo wa kisiasa unaounganisha nchi nane za kanda ya Maziwa Makuu ya Afrika Mashariki: Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Somalia[2], Sudan Kusini[3], Tanzania na Uganda.[4]
Ukweli wa haraka Lugha rasmi, Viongozi ...
Jumuiya ya Afrika Mashariki English: East African Community |
||||||
---|---|---|---|---|---|---|
Wito: Taifa Moja Mustakabali Mmoja English: "One People One Destiny" |
||||||
Wimbo wa taifa: Jumuiya Yetu | ||||||
Makao makuu | Arusha, Tanzania | |||||
Lugha rasmi | Kiswahili, Kiingereza | |||||
Aina | Shirika la kimataifa | |||||
Uanachama | Burundi Kenya Democratic Republic of the Congo Rwanda Somalia South Sudan Tanzania Uganda |
|||||
Viongozi | ||||||
- | Mwenyekiti | Salva Kiir Mayardit | ||||
- | Mwenyekiti wa Baraza | Shem Bageine | ||||
- | Rais wa Mahakama | Harold Nsekela | ||||
- | Spika wa Bunge | Margaret Zziwa | ||||
- | Katibu Mkuu | Richard Sezibera | ||||
Bunge | Bunge la EAC (EALA) | |||||
Maanzilisho | ||||||
- | Mara ya kwanza | 1967 | ||||
- | Kufutwa | 1977 | ||||
- | Mara ya pili | 7 July 2000 | ||||
Eneo | ||||||
- | Jumla | 4,810,363 km2 (7th a) 1,857,292 sq mi |
||||
- | Maji (%) | 4.14 | ||||
Idadi ya watu | ||||||
- | 2022 makisio | 312,362,653 a (4th) | ||||
- | Density | 58.4/km2 151.3/sq mi |
||||
Pato la Taifa | makisio 2020 | |||||
- | Total | US$ 602.584 billion[1] (34tha) | ||||
- | Per capita | US$ 3,286 | ||||
GDP (nominal) | 2020 estimate | |||||
- | Total | US$ 220.783 billion (50tha) | ||||
- | Per capita | US$ 1,185 a | ||||
Currency | 5 Currenciesb Kigezo:Currency table |
|||||
Saa za eneo | CAT / EAT (UTC+2 / +3) | |||||
Tovuti eac.int |
||||||
a. | If considered as a single entity. | |||||
b. | To be replaced by the East African shilling |
Funga
Kwa sasa eneo la Mtangamano ni km2 4,810,363, likiwa na wakazi 312,362,653 (kadirio la mwaka 2022), hivi kwamba ingekuwa nchi moja tu ingekuwa ya nne duniani.
Jumuiya yenye jina hilo imepatikana mara mbili katika historia: jumuia ya nchi tatu kati ya hizo ilianzishwa mwaka 1967, lakini ilisambaratika mwaka 1977[5][6][7] ikafufuliwa rasmi tarehe 7 Julai 2000.[8]