Julia Salzano
From Wikipedia, the free encyclopedia
Julia Salzano (Santa Maria Capua Vetere, Caserta, 13 Oktoba 1846 – Casoria, Napoli, 17 Mei 1929) alikuwa sista wa Kanisa Katoliki nchini Italia na mwanzilishi wa shirika la Masista wa Katekesi wa Moyo Mtakatifu wa Yesu (21 Novemba 1905) kwa ajili ya kufundisha imani na maadili ya Kikristo na kueneza ibada kwa ekaristi takatifu[1].
Kabla ya kuwa mtawa, Julia Salzano alikuwa mwalimu na kuanzia mwaka 1865 alifanya kazi Casoria alipojitokeza kama katekista bora pia.[2][3]
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 27 Aprili 2003, halafu Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu tarehe 17 Oktoba 2010.