Jermano wa Paris
From Wikipedia, the free encyclopedia
Jermano wa Paris (Autun, leo nchini Ufaransa, 496 hivi - Paris, 28 Mei 576) alikuwa mmonaki ambaye, baada ya kuwa abati wa monasteri karibu na Autun, alichaguliwa kuwa askofu wa Paris akafanya uchungaji bila kulegeza maisha magumu aliyozoea[1].
Venansi Fortunati alimsifu sana katika kitabu alichoandika juu yake[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.