Isaka Jogues
From Wikipedia, the free encyclopedia
Isaka Jogues, S.J. (Orleans, Ufaransa 10 Januari 1607 – Ossernenon, Marekani, 18 Oktoba 1648) alikuwa padri Mjesuiti ambaye mwaka 1636 alijiunga na wamisionari kwa Waindio wa Amerika Kaskazini[1] akauawa nao kwa ajili ya imani yake.
Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930[2].