Hugo wa Lincoln
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hugo wa Lincoln, O.Cart. (pia: Hugo wa Avalon; Avalon[1], Dauphiné, Ufaransa Kusini, 1135/1140 – London, Uingereza, 16 Novemba 1200) alikuwa padri Mwaugustino, halafu mmonaki Mkartusi. Alitumwa kuongoza monasteri ya kwanza ya shirika lake Uingereza mwaka 1179[2].
Mwaka 1186 alifanywa askofu wa Lincoln [3].
Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waanglikana kama mtakatifu tangu alipotangazwa na Papa Honori III tarehe 17 Februari 1220.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 17 Novemba[4].