Hubertus wa Liege
From Wikipedia, the free encyclopedia
Hubertus au Hubert (656 hivi – Tervueren, leo nchini Ubelgiji, 30 Mei 727) alikuwa askofu wa Tongeren-Maastricht, kati ya Ubelgiji na Uholanzi kuanzia mwaka 708[1].
Mwanafunzi na mwandamizi wa Lambati wa Maastricht, aliinjilisha kwa bidii eneo hilo na kung’oa mila za Kipagani hata akapewa jina la Mtume wa Ardennes[2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waanglikana kama mtakatifu.[4]