Guntram
From Wikipedia, the free encyclopedia
Guntram (pia: Gontran, Gontram, Guntram, Gunthram, Gunthchramn, Guntramnus; Soissons, Aisne, leo nchini Ufaransa, 532 hivi - Chalon-sur-Saône, leo nchini Ufaransa, 28 Machi 592) alikuwa mfalme wa Wafaranki huko Orleans na Burgundy tangu mwaka 561[1][2].
Alikuwa na tabia mbaya na kutenda dhambi nyingi, lakini imani ilimuongoza kuheshimu Kanisa na viongozi wake, kujenga monasteri na kuhamasisha uinjilishaji, kupatanisha ndugu zake[3], kusaidia maskini na kuwaombea kwa kufunga mwenyewe[4].
Kwa sababu hiyo tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.