Geronsi wa Cervia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Geronsi wa Cervia (alifariki Cagli, Marche, Italia ya Kati, 501/504) alikuwa askofu wa kwanza anyejulikana wa Cervia, Italia Kaskazini[1] aliyeshiriki sinodi huko Roma na kumuunga mkono Papa Simako dhidi ya antipapa[2].
Aliuawa njiani, lakini sababu zinazotolewa ni tofautitofauti.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, pengine pia mfiadini.