Gaspare Bertoni
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gaspare Bertoni (9 Oktoba 1777 ā 12 Juni 1853)[1] alikuwa padri Mkatoliki wa Verona (Italia) aliyeanzisha shirika la Wastigmatini ambalo limeenea hata Tanzania. Lengo lake lilikuwa kuandaa wamisionari walio tayari kutumikia maaskofu.
Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 1 Novemba 1975, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 1 Novemba 1989.