Gabrieli Lalemant
From Wikipedia, the free encyclopedia
Gabrieli Lalemant, S.J. (Paris, Ufaransa 3 Oktoba 1610 ā Waubaushene, karibu na Tay, Ontario, Kanada, 17 Machi 1649) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari mwenye bidii ya ajabu kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1646, aliyewatangazia utukufu wa Mungu kwa lugha yao[1].
Alikamatwa pamoja na Waindio hao[2], akateswa sana akauawa na Wairoki, kabila lingine la Waindio.
Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930[3].
Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].