Fransisko Antoni Fasani
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fransisko Antoni Fasani (Lucera 6 Agosti 1681 - Lucera 29 Novemba 1742) alikuwa padri wa utawa wa Ndugu Wadogo Wakonventuali kutoka Italia Kusini.
Msomi mkubwa, alipenda sana kuhubiri na kufanya toba, pamoja na kuhurumia fukara kwa kuwapa hata mavazi yake.
Alitangazwa na Papa Pius XII kuwa mwenye heri tarehe 15 Aprili 1951, halafu tarehe 13 Aprili 1986 Papa Yohane Paulo II alimtangaza kuwa mtakatifu.