Fokas wa Sinope
From Wikipedia, the free encyclopedia
Fokas wa Sinope (alifariki Sinope, leo nchini Uturuki, 300 hivi) alikuwa mtunzabustani ambaye alitumia mazao yake kulisha fukara na Wakristo walioteswa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma[1]. Mwishoni hata yeye aliuawa kikatili kwa imani ya Kikristo [2][3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini[4].