Emilia wa Vialar
From Wikipedia, the free encyclopedia
Emilia wa Vialar (kwa Kifaransa Émilie de Vialar, 12 Septemba 1797 – 24 Agosti 1856) alikuwa mtawa Mfaransa aliyeanzisha na kueneza kwa bidii shirika la kimisionari la Masista wa Mt. Yosefu wa Njozi kutoka Ulaya hadi Afrika, Asia na Australia[1].
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu. Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI tarehe 18 Juni 1939, halafu mtakatifu na Papa Pius XII tarehe 24 Juni 1951.