Emerensyana wa Roma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Emerensyana wa Roma (alifariki Roma, Italia, 304 hivi) alikuwa na undugu[1][2] na Agnes wa Roma, bikira mwenye umri wa miaka 12 ambaye alikataa kuolewa kwa sababu ya imani yake ya Kikristo na kwa sababu hiyo aliteswa akauawa wakati wa dhuluma ya Dola la Roma dhidi ya Wakristo.
Siku chache baadaye, Emerensyana, ambaye alikuwa anajiandaa kubatizwa, alikwenda kwenye kaburi la Agnes, kumbe alishambuliwa na kuuawa kwa mawe na umati wa Wapagani.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake ni tarehe 23 Januari[3].