Edmund Rich
From Wikipedia, the free encyclopedia
Edmund Rich (Abingdon, Uingereza, 1174 hivi – Soisy-Bouy, Ufaransa, 16 Novemba 1240) alikuwa mwalimu maarufu wa hisabati, falsafa na teolojia katika vyuo vikuu vya Paris na Oxford, halafu mhubiri, na hatimaye askofu mkuu wa Canterbury.
Kwa juhudi zake alirekebisha umonaki, Kanisa la Uingereza na nchi kwa jumla[1].
Alitangazwa mtakatifu na Papa Inosenti IV tarehe 16 Desemba 1246.
Wakatoliki[2] na Waanglikana wanaadhimisha sikukuu yake tarehe ya kifo chake.