Devota wa Mariana
From Wikipedia, the free encyclopedia
Devota wa Mariana (Lucciana, Corsica, leo nchini Ufaransa, 283 - Mariana, Corsica, 304) alikuwa Mkristo bikira aliyefia imani yake katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 27 Januari[2].