Bruno wa Querfurt
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bruno wa Querfurt, O.S.B.Cam. (Querfurt, leo katika Saxony-Anhalt, Ujerumani, 974 hivi – Moravia Mashariki, 14 Februari au 9/14 Machi 1009) alivutiwa na karama ya Romwaldo akaamua kuwa mmonaki wa urekebisho wa Wabenedikto wa Camaldoli alipofika Italia kuongozana na kaisari Oto III. [1]
Aliporudi Ujerumani alifanywa askofu na Papa Yohane X. Katifa safari ya kimisionari aliuawa na Wapagani pamoja na wenzake 18 huko Ulaya mashariki (kati ya Lituania na Ukraina).
Tangu kale Bruno na wenzake wanaheshimiwa kama watakatifu.