Brisi wa Tours
From Wikipedia, the free encyclopedia
Brisi wa Tours (Turenne, 370 hivi- Tours, leo nchini Ufaransa, 444 BK) alikuwa askofu wa mji huo kwa miaka 47 baada ya mwalimu wake Martino wa Tours (397) [1] .
Gregori wa Tours aliandika maisha yake[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Novemba[3].