Birinus
From Wikipedia, the free encyclopedia
Birinus (600 hivi – 649) alikuwa mmonaki wa Kikolumbani aliyefanywa askofu wa kwanza wa Dorchester[1].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu na kuitwa "mtume wa Wasaksoni wa Magharibi" kutokana na kuingiza ufalme wa Wessex katika Ukristo.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 3 Desemba[2] au 4 Septemba.