Benyamini wa Argol
From Wikipedia, the free encyclopedia
Benyamini wa Argol (alifariki Argol, nchini Uajemi, 424 hivi) alikuwa shemasi aliyeteswa na kuuawa kwa sababu aliendelea kuhubiri imani yake katika dhuluma ya mfalme Vararane V[1][2]. Walimuingizia ncha kali katika makucha yake.
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.