Benwadi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Benwadi wa Hildesheim (jina asili: Bernward; 960 – 20 Novemba 1022) alikuwa askofu wa Hildesheim nchini Ujerumani kuanzia tarehe 15 Januari 993 hadi kifo chake[1] [2].
Benwadi aliagiza ujenzi wa kanisa kubwa la Mt. Mikaeli kwa mtindo wa Kiroma na pia kutengenezwa kwa milango ya shaba kwa kanisa kuu la Hildesheim; yote mawili yametambuliwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia[3].
Papa Selestini III alimtangaza mtakatifu tarehe 19 Desemba 1192.
Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Waorthodoksi tarehe 20 Novemba[4].