Benedikto wa Aniane
From Wikipedia, the free encyclopedia
Benedikto wa Aniane, O.S.B. (jina la kuzaliwa Witiza; huitwa pengine Benedikto wa pili; 747 hivi ā 12 Februari 821) alikuwa mmonaki na mrekebishaji wa Utawa wa Mt. Benedikto, ambaye aliathiri sana hali ya Kanisa katika dola la Karolo Mkuu pia kwa kurekebisha liturujia ya Roma.
Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.