Ardabil
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ardabil (pia Ardabīl na Ardebīl , Kiajemi na Kiazeri : اردبیل) ni mji wa kihistoria kaskazini-magharibi mwa Iran. Jina Ardabil linatokana na jina la Kiajemi cha kale "Artawila", likimaanisha mahali patakatifu. [1] Ardabil ni makao makuu wa Mkoa wa Ardabil . Katika sensa ya 2011, idadi ya wakazi ilikuwa 564,365 katika familia 156,324, Wakazi wengi ni Waazeri. [2] [3] Ardabil pia inajulikana kwa patakatifu na kaburi la Safî ad-Dîn na jina lake lilikuwa chanzo cha nasaba ya wafalme wa Safavi .